SIMULIZI;MKATABA
WA DAMU
MWANDISHI;
SANTOS AMANI MWAKOMO
PHONE;
0742516353
MWANZO
KIshindo
kikubwa kilisikika kwenye barabara ya sam nujoma huku kila mmoja akiwa haamini
jambo lililotokea wakatii huo, katika barabara hio. Ilikua ni ajali mbaya sana iliyohusisha
gari la mafuta la kampuni ya fast oil pamoja na gari dogo binafsi aina ya
Subaru legacy. Mashuhuda walisogea kwa kasi eneo la tukio huku wakimzonga
dereva wa gari la mafuta ambaye aliruka upande wa pili na kukimbia ili apate
kuokoa roho ake kutoka kwa watu wenye hasira kali.
Katika hali
isiyo ya kawaida gari la mafuta lilianza kuvuja mafuta na kuwafanya watu waanze
kusogea na vyombo vya kukingia mafuta ili waweze kupata ridhiki kila mtu kwa
wakati wake.
Hakuna
aliyejali tena kuhusu watu waliokua kwenye gari dogo kila mtu alikua bize
kukinga mafuta na wachache walikua wakipiga picha za tukio zima.
Dakika kumi
baada ya ajali hio vilio vilisikika huku anga la eneo hilo likitawaliwa na
moshi mzito uliosababishwa na mlipuko mkubwa wa gari la mafuta, watu walikimbia
kwa pupa huku kila mtu akijaribu kuokoa nafsi yake kwa wakati wake na wakati
huo gari dogo lilionekana kuteketea huku kukiwa hakuna mtu aliyejaribu
kulisogelea.
Jeshi la
polisi pamoja na zima moto waliwasili
punde bada ya mlipuko huo huku wakijaribu kuzima moto na kuokoa wahanga
waliokumbwa na janga hilo, walifanya kadiri wawezavyo kuokoa majeruhi pamoja na
watu waliokumbwa na umauti baada ya ajali hio ambapo zoezi hilo lilidumu kwa
takribani dakika arobaini na tano huku waandidhi wa habari nao wakirekodi tukio
zima mubashara.
Taarifa hizo
zilimfikia bi grace warioba, mke wa james warioba akiwa nyumbani kwake
mikocheni ambaye awali alikua hana shaka juu ya taaifa ile lakini kadiri
msomaji alipokua akiendelea kutoa taarifa ya habari ndivyo moyo wake ulivyozidi
kwenda mbio.
Hakuweza
kuvumilia aliamua kumpigia simu ramsey mtoto wake wa kwanza lakini hakikuweza
kupatikana, alimpigia tricia ambaye simu yake iliita bila kupokelewa na haimaye
ikawa haipatikani kabisa.
“ee mungu
wangu wasiwe wanangu kwenye ajali hio”. Aliongea bi grace na kuchukua biblia
apate kusoma mistari yenye kumpa nguvu kidha baada ya muda alijaribu kupiga
tena simu lakini majibu yalikua yale yale
Wazo
lililomjia kichwani ni kumpigia mumewe james warioba apate kujua kama alikua na
mawasiliano na wanae kwani moyo yake hakua na amani kabisa, simu iliita ana
kupokelewa
“naam mke
wangu”. aliongea james kwa utulivu wa hali ya juu
“moyo wangu
umekufa ganzi, sina amani kabisa nahisi huenda kuna jambo baya linakwenda
kutokea”. Aliongea bi grace
“hapana mama
tumuombe mungu atuepushie matatizo katika familia yetu, lakini unajua nini mke
wangu……”. aliongea james warioba lakini kabla hajamaliza kuzungumza aliona
taarifa ya habari kwenye luninga iliyotangaza kuhusu ajali iliyolihusisha gari
lake dogo aina ya Subaru legacy 2019 ambalo alilinunua kama zawadi kwa mwanae
ramsey baada ya kuhitimu mafunzo ya udaktari wa moyo nchini china.
James
warioba alishindwa kuongea tena na kukata simu, kisha kuondoa gari haraka na
kwenda nyumbani kisha kumchukua mkewe ambapo walikwenda moja kwa moja eneo la
tukio.
Hakika bi
grace hakuweza kuamini kwamba ni wanae ndio walioteketea ndani ya gari baada ya
ajali ile ambayo pia iliua takribani raia sabini (70).
James
aliumia sana lakini alikua na kazi ya kumtuliza mkewe ambaye alilia hadi
kupoteza fahamu, hakika kilikua ni kipindi kigumu sana kwa upande wa james
warioba kwani hata miili ya watoto wahe haikuweza kuonekana baada ya kuteketea kwa moto.
Maombolezo
ya kitaifa yalifanyika na baada ya muda kupita taratibu jambo hilo lilipita
huku kila mmoja akiacha kuizungumzia ajali hio ambayo wengine walidai ni kafara
na watu walitoa mitazamo tofauti kila mtu alivojisikia kuzungumza.
Picha wa
wanae na matukio ya furaha yalikua yakijirudia kichwani mwa bi grace na kumfanya
alie muda wote huku akimlaumu mungu kwa kuwachukua watoto wake wakiwa na umri
mdogo kabisa.
“mke wangu,
hupaswi kua unalia kila wakati kazi yake mola haina makosa”. Aliongea james
“inauma sana
mume wangu, sasa na uzee huu tutapata wapi watoto” aliongea bi grace kwa
uchungu sana jambo ambalo lilimuumiza sana james lakini hakua na budi kuitunza
siri ya mkataba wa damu moyoni mwake kwani angekufa endapo angeitoa.
“akili, na
moyo wangu vinaniambia kwamba wanangu bado wapo hai na wanaishi kwenye
ulimwengu wa mateso sana kwani vifo vyao havikupangwa na mola”. Aliongea bi
grace na kumfanya james apate mstuko huku moyo wake ukimpasuka
“paaah”.
“ila unajua
mke wangu, tuache kuyaongea hayo mambo mimi naogopa sana usiku”. Alijitetea
james huku akimshinikiza mkewe wakapumzike chumbani.
“kazi nzuri
sana umeifanya mr james, tunakutunuku pete ya utajiri kampuni yako itapata
faida mara kumi zaidi ya awali, hakikisha haioni mtu yoyote, umesaini mkataba wa damu”.
James
alistuka kutoka usingizini ambapo alijikagua kwenye vidole vya mikono yake, na
kukutana na pete yenye rangi ya bluu na nakshi za almasi huku akihema kwa nguvu
aliinuka kitandani kisha alinyata kuelekea nje, lakini kabla hajafungua mlango
mkewe alimwita.
Je nini
kilifuata?
nzuri
JibuFuta