SIMULIZI;MKATABA WA DAMU MWANDISHI; SANTOS AMANI MWAKOMO PHONE; 0742516353 MWANZO KIshindo kikubwa kilisikika kwenye barabara ya sam nujoma huku kila mmoja akiwa haamini jambo lililotokea wakatii huo, katika barabara hio. Ilikua ni ajali mbaya sana iliyohusisha gari la mafuta la kampuni ya fast oil pamoja na gari dogo binafsi aina ya Subaru legacy. Mashuhuda walisogea kwa kasi eneo la tukio huku wakimzonga dereva wa gari la mafuta ambaye aliruka upande wa pili na kukimbia ili apate kuokoa roho ake kutoka kwa watu wenye hasira kali. Katika hali isiyo ya kawaida gari la mafuta lilianza kuvuja mafuta na kuwafanya watu waanze kusogea na vyombo vya kukingia mafuta ili waweze kupata ridhiki kila mtu kwa wakati wake. Hakuna aliyejali tena kuhusu watu waliokua kwenye gari dogo kila mtu alikua bize kukinga mafuta na wachache walikua wakipiga picha za tukio zima. Dakika kumi baada ya ajali hio vilio vilisikika huku anga la eneo hilo likitawaliwa na moshi mzito uliosababishw...